19 Machi 2015 - 19:20
 Kasri la rais lashambuliwa Aden Yemen

Ndege ya kivita isiojulikana imeshambulia kasri la rais mjini Aden leo hii baada ya vikosi tiifu kwa Rais Abd Rabbu Mansour Hadi kushambulia kambi moja ambako kamanda muasi alikuwa amejifungia.

Ndege ya kivita isiojulikana imeshambulia kasri la rais mjini Aden leo hii baada ya vikosi tiifu kwa Rais Abd Rabbu Mansour Hadi kushambulia kambi moja ambako kamanda muasi alikuwa amejifungia.

Ndege hizo zilidondosha bomu na zilifyatuwa makombora katika uwa wa kasri hilo lilioko katika kitongoji cha al-Maasheeq kwenye mji huo wa bandari ambako ndiko anakoishi Hadi.Kwa mujibu wa mashahidi mizinga ya kutungulia ndege ilifyatuliwa dhidi ya ndege hizo na moshi ulikuwa umetanda kwenye eneo hilo.Duru za usalama zinasema hali katika kasri hilo la rais imedhibitiwa na hakuna cha kuhofia.Inaelezwa kwamba Hadi mwenyewe hakudhurika na yuko mahala salama na kwamba hakuondoka nchini humo.